Kazi Kazi’ Ndiyo Ujio Mpya Prof Jay Kwenye Game
Mbunge wa jimbo la Mikumi kupitia tiketi ya Chadema na mwanamuziki wa Hip hop Prof Jay amefunguka na kusema kuwa amendika na kutengeneza video ya wimbo wake mpya alioupa jina la ‘Kazi kazi’ ili kuwatia moyo vijana na watu waliokata tamaa ya maisha na kuwataka kufanya kazi kwani ipo siku maisha yao yatabadilika.
Prof Jay amesema wimbo wake huo mpya ameamua kwenda kutengeneza video yake Manzese katika uwanja wa Fisi ili kuwapa matumaini mapya na nguvu kwa watu waliokata tamaa ya maisha.
“Kwa heshima kubwa sana tumeshoot video hii maeneo ya Manzese uwanja wa fisi, tukiwapa tumaini jipya na nguvu wale wote waliokata tamaa na kuwaambia wakomae kwa kufanya kazi kwani ipo siku mambo yatakuwa sawa” alisema Prof Jay
Mbali na hilo Prof Jay amesema wimbo huo amemshirikisha msanii Sholo Mwamba ambaye ambaye anafanya muziki aina ya singeli, huku wimbo huo ukiandaliwa na producer Mensen Selekta huku video hiyo ikiandaliwa na muongozaji wa video ambaye kwa sasa anafanya vizuri Travellah kutoka ‘Kwetu studio’
eatv.tv