Kesi ya Masogange Yapigwa Kalenda
Kesi inayomkabiri mrembo Agnes Gerald maarufu kama Masogange imeahirishwa hadi Agosti 2 mwaka huu, kesi hiyo imepigwa kalenda kutokana na Wakili wa Serikali kuuguliwa na mtoto wake.
Masogange ambaye amejizolea umaarufu nchini kutokana na kupamba video za wasanii mbalimbali, anakabiliwa na mashitaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.
Katika kesi hiyo namba 77 ya mwaka 2017, Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14, mwaka huu, katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine) na kati ya Februari 7 na 14, 2017 alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.
Bongo5