Artists News in Tanzania

Khadija Kopa Afunguka Kutaka Kuolewa

Malkia wa Mipasho nchini Tanzania asiyekuwa na mshindani, Khadija Kopa ametangaza rasmi kuhitaji mume wa kumuoa ili aweze kuishi naye huku akiweka vigezo vyake kuwa hataki aliyechini ya miaka 40 kwa madai hawezi kufundisha tution.

Khadija Kopa ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI cha  EATV.

“Sijaolewa ila sitaki kusomesha tuition, nataka mwanaume aliyekuwa na umri mkubwa kuanzia 40 kwenda juu, mwenye mapenzi ya dhati na huba, mwenye kujali na kujua ninataka nini, atakayeweza kuijali familia yangu pamoja na watoto wangu, awe mnene kidogo na sio mwembamba, awe na rangi yeyote na kabila lolote lile kwasababu mimi sina ubaguzi katika vitu hivyo”, amesema Khadija Kopa.

Pamoja na hayo, Khadija Kopa ameendelea kwa kusema “napenda mwanaume mfanyakazi maana kupata pesa ni majaliwa ila asiwe mwanaume wa kulala nyumbani akanitegemea mimi nikafanye kazi ili yeye aje kula maana maisha ni kusaidia nasio kuegemea upande mmoja tena wa mwanamke”.

Aidha, Khadija Kopa amesema sababu kubwa iliyompelekea mpaka sasa kutoolewa ndoa nyingine baada ya aliyekuwa mume wake kufariki ni kutokana na kuwa na wasiwasi na wanaume wa sasa.

“Nina wasiwasi kwa mwanaume atakayekuja kunioa kwa sasa, maana najiuliza mengi je atakuwa na huba kama marehemu mume wangu ndio maana mpaka sasa sijaolewa kwa kuwa nafikiria sana. Mume wangu aliyefariki alikuwa ni mwenye huba, mwenye kunijali, nimekaa naye miaka yote sijawahi kugombana naye, nilikuwa natamani kumuona akinuna ananuna vipi, alikuwa na vigezo vyote”, amesisitiza Khadija Kopa.

EATV.TV

Comments

comments

Exit mobile version