Kigwangalla Akifunga Kiwanda cha Afro-American Kinachozalisha Viroba Feki
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla, ameendelea na usimamizi wa Operesheni Maalum ya kufuatilia na kuufumua mtandao wa Viroba na Pombe feki na haramu nchini.
Mchana huu amelazimika ku na vinginevyo ambavyo vimekutwa havina vibali vya TFDA na havina usajili wa TFDA, havina Batch Number ya kutambua uhalali wa uzalishaji wake, havina tarehe ya kuzalishwa na wala ya ku-expire. Hivyo ni ngumu kutambua ubora wake na idadi yake halisi kwa maksudi ya kulipa kodi ya serikali.
Wenye kiwanda hawatunzi rekodi za uzalishaji na wamekiri kuwa mitambo yao haina uwezo wa kuweka batch number.
Jana akiendesha operesheni hii maalum, Dkt. Kigwangalla alibaini uwepo wa bidhaa hizi sokoni na hivyo aliagiza wataalamu wafuatilie kinyume nyume kujua zinakotoka. Upelelezi umewafikisha hapa.
Chanzo:GPL