Mke wa muongozaji wa Filam Tanzania Gift John Lister aliyefariki wiki iliyopita akiwa anasumbuliwa na homa ya mapafu amezikwa Jumamosi hii katika makaburi ya Kinindoni.
Akiongea kupitia eNewz mume wa marehemu Director John Lister amesema marehemu ameacha watoto wawili na siku tatu zilizopita waligundua kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na homa ya mapafu na wakati anapatiwa matibabu ndipo umauti ukamfika.
Pia John Lister amewashukuru wasanii wote pamoja na marafiki waliojitokeza katika mazishi ya mke wake, bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe
eatv.tv
Comments
comments