Msanii wa filamu wa Tanzania Jacob Steven amesema kifo cha Kanumba kilitokea wakati yupo kwenye ‘pick’ kwenye sanaa yake, na kufanya kuonekana wengine waliobaki hawana uwezo zaidi yake.
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Rdio, JB amesema si kama Kanumba hakuwa muigizaji mzuri, au hakukuwa na waigizaji wazuri zaidi yake, isipokuwa alifariki katika kipindi ambacho yeye ndiye alikuwa anawika, kitu ambacho ni sawa na kilichotokea na Bob Marley.
“Sio kama hakukuwa na waigizaji wazuri zaidi ya Kanumba, lakini pia si kama Kanumba hakufanya vizuri, Kanumba aliweka nguvu zake zote kwenye sanaa, lakini kilichotokea ni kwamba Kanumba alifariki akiwa katika ‘pick’, kama Bob Marley, leo inaonekana hakuna mwanamuziki bora wa reggae zaidi yake. Kuna Bruce Lee, leo Jackchain anafanya vitu vikubwa kuliko Buce lee, lakini watu watakwambia sio kweli, kuna idea kwamba mtu akifariki akiwa kwenye pick ni ngumu sana kusema kuna mtu atamzidi”, amesema JB.
Kauli hiyo ya JB imefuatia baada ya malalmiko mengi kwamba sanaa ya filamu bongo imekufa baada ya kifo cha Kanumba, na ndipo akatolea ufafanuzi huo na kusema sio kweli kwamba bongo movie imekufa na Kanumba.
Comments
comments