King Majuto: Baada ya Ramadhani Anakuja Nahii
MSANII mkali wa filamu, maigizo na vichekesho nchini, Amri Athuman maarufu King Majuto, anatarajia kutambulisha filamu yake mpya itakayojulikana kwa jina la ‘Uganga Basi’.
Mkali huyo ambaye kwa sasa anatamba na filamu yake mpya inayoitwa ‘Kirungu’ aliyomshirikisha mchekeshaji mahiri na mkongwe katika vichekesho, Brother K, alisema filamu hiyo itatoka Julai mwaka huu.
Majuto aliliambia MTANZANIA kwamba filamu hiyo ina mafunzo ya kutosha huku akiamini itatoa mafunzo mengi kuhusiana na uganga unaotumikiwa na wengi na kusahau mambo mengine ya maendeleo,” alisema.