King Majuto Kuja na Lakuvunda
AMRI Athuman ‘King Majuto’ baada ya kutoka Hija anatarajia kuja na filamu kali ya Lakuvunda ambayo itakuwa ni funga mwaka 2015, sinema hiyo ambayo imetengenezwa katika kiwango cha kimataifa, akiongea FC msemaji wa kampuni ya Splash Entertanment Steve Selenge amesema ni kazi nzuri.
“Filamu ya Lakuvunda imetengenezwa katika kiwango cha hali ya juu sana maana ni kazi ya kufunga mwaka kuanzia ubora wa hadithi production na waigizaji hasa King Majuto amefunika,”anasema Selenge.
Sinema ya Lakuvunda inatarajia kutoka wiki ijayo tarehe 21. December.2015 siku ya jumatatu katika sinema hiyo wapo wasanii wakali kama King Majuto, Riyama Ali, Asha Boko, Tausi Mdegela na wasanii wengine wanaofanya vema katika tasnia ya filamu.
FC