Msanii wa vichekesho na muimbaji, Kingwendu amesema angependa kuwa na msimamizi wa shughuli zake katika sanaa ya muziki ili aweze kutoka badala ya kutegemea uchekeshaji peke yake.
Msanii wa vichekesho na muimbaji, Kingwendu amesema angependa kuwa na msimamizi wa shughuli zake katika sanaa ya muziki ili aweze kutoka badala ya kutegemea uchekeshaji peke yake.
Akizungumza na Times Fm, Kingwendu alisema kuwa amekuwa akitoa nyimbo mbalimbali lakini bahati mbaya hazipati nafasi ya kusikilizwa kwenye vituo vya redio kwa ajili ya kumtangaza.
“Nimegundua kuwa sababu kubwa ambayo inanikwamisha kutoka kimuziki ni kukosa meneja wa kusimamia kazi zangu, hivyo najaribu kuangalia uwezekano wa kumpata,” alisema kingwendu.
Msanii huyo alisema kuwa ana uwezo wa kupambana na wasanii wa muziki wa kizazi kipya wanaotamba kwa sasa na kuwabwaga iwapo atapata meneja wa kusimamia kazi zake vizuri.
“Hao wanaotamba sasa ni kwa sababu wana watu wa kusimamia kazi zao na mimi nitafanya hivyo ndipo mtaamini kile ninachokisema kwamba nina uwezo mkubwa wa kuimba ila ninakosa usimamizi tu,” alisema
Comments
comments