Tangu malkia wa filamu nchini, Wema Sepetu aachane na mpenzi wake Idris Sutlan kuna mengi yamekuwa yakizungumzwa katika mitandao ya kijamii.
Muigizaji huyo hakuwahi kuzungumza sababu ya kuachana na mshindi huyo wa shindano la Big Brother Africa Hotshots 2014 hali ambayo imekuwa ikiibua maswali mengi kwa mashabiki wake.
Alhamisi hii Wema amewataka mashabiki wake katika mitandao ya kijamii kukaa mkao wa kula kwa ajili ya kuyasikia mengi ambayo yanaukabili moyo wake.
“Kuna muda mtu unaweza ukakaa na ukasema na moyo wako, Ila moyo mara nyingi huwa unazidi nguvu nyingine zozote. Kuna kitu kiukweli ninacho kwa moyo wangu,” aliandika mwigizaji huyo kupitia ukurasa wa instagram.
Aliongeza, “Lakini siwezi kusema leo wala kesho, but ipo siku isiyo na jina wala tarehe nitakisema tu, maana mnanijua kukalfisha nafsi huwa sipendi, but all in all tuseme Inshallah,”
Wiki iliyopita aliyekuwa mpenzi wake, Idris Sultan aliamua kufuta akaunti yake ya instagram yenye followers zaidi ya milioni 1 baada ya kushindwa kuvumilia yale yanayoendelea katika mitandao ya kijamii.
Comments
comments