Kuna Wasanii Wanabebwa na Media – Roma
Msanii wa hip hop Bongo, Roma amekiri kuwa kuna baadhi ya wasanii wanapata upendeleo wa ngoma zao kupata airtime katika media.
Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Zimbabwe’ ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa mara nyingi siyo kitu kizuri kwani pale msaada huo unapofika kikomo msanii hupotea kwenye muziki.
“Yeah, off course asilimia mia moja kuna wasanii wanabebwa na media na pale media inapokata mirija utaona the way wanavyoshindwa kuishi kitu ambacho si kizuri, nashauri mtu atumie kipaji chake halafu aweze kujua at any time unaweza ukabwagwa na media halafu ukatakiwa usimame wewe kama wewe sasa kitaa unacho?, kwa sababu mimi naamini cha kwanza kitaa,” amesema na kuongeza.
“Kitaa kikikuelewe media ni bless tu, utakuta ni Miaka minne/mitano wimbo wangu haujaingia kwenye chart za top ten lakini nikidondoka kwenye show na huo wimbo, bwana wee!!, kwa hiyo ile show yangu ya Mbagala ndio top ten yangu” amesisitiza.
Bongo5