KUONDOA VITU VISIVYO NA UMUHIMU NA KUSAIDIA WENYE UHITAJI
KUONDOA VITU VISIVYO NA UMUHIMU NA KUSAIDIA WENYE UHITAJI.
Kuhusu sisi.
Kampeni ya kuondoa vitu visivyo na umuhimu ni jitihada ya wajibu wa kijamii inayowataka wananchi kuchangia vitu vyao vya ziada ili kuwasaidia wahitaji.
Lengo la kampeni
Lengo la kampeni hii ni kuibua uelewa kuhusu hasara za kurundika vitu visivyokuwa na umuhimu, faida za kuviondoa vitu hivo na jinsi vinavyoweza kutumika katika maisha yetu ili kupata fedha za kuwasaidia wahitaji. Tunakusudia kupata fedha kutokana na mauzo ya Vifaa vlivyopo katika maghala kwa ajili ya kupat fedha kuwasaidia makundii ya wahitaji.
Walengwa
Tunakusudia kusaidia vituo vya watoto yatima kwa kuwapatia vitabu na michezo ya watoto.
Pia tunakusudia susaidia wanawake wanaoishi katika mazaingira magumu kwa kuwapatia elimu ya hedhi salama na kuwapatia vifaa vy akujihifadhi.
Kampeni hii ina vipengele 3;
1. Makusanyo na Elimu
Uhamasishaji , utoaji wa elimu kuhusu madhara ya kujirundikia vitu naukusanyaji wa vitu kutoka kwa watu binafsi na taasisi mbalimbali kuanzia tarehe 25.09.2016 – 04.12.2016.
2. Yard Sale
Mauzo ya vitu vilivyokusanywa yatafanyika tarehe 10.012.2016
3. Utoaji wa Misaada
Semina hukusu hedhi salama na ugawaji wa taulo za kina mama itafanyika tarehe 15.012.2016. Utoaji wa msaada katika kituo cha watoto yatima utafanyika tarehe 20.12.2016
Wasiliana nasi:
Simu: +255 682 969 890 | Barua pepe: declutteranddonate@eliteorganizers.com
Facebook: | Instagram: @declutteranddonate | Twitter: @DeclutterTZ