Moja habari zilizoandikwa ni hii habari kwenye gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Miamala ya simu bei mpya balaa’
Wakati Serikali ikisema uanzishaji wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT), kwenye miamala ya simu na benki haitawahusu wateja, kampeni za simu zimepandisha mara dufu gharama za kutuma na kupokea fedha.
Tofauti na benki ambazo zinatoa matangazo kwa umma juu ya kupandisha gharama miamala na huduma zake kabla ya mwaka wa bajeti wa 2016/17 kuanza, kampuni za simu zimepandisha gharama bila kutoa taarifa kwa umma.
Kutokana na tangazo la benki la hizo, tangu julai mosi watumiaji wa huduma za kibenki walitarajiwa kuanza kukatwa asilimia 18 ya kodi ya VAT katika kila muamala wanaoufanya ambazo ni kati ya sh. 152.50 katika kila mapato ya sh. 1000 yanatozwa na benki, mteja anapofanya muamala.
Baada ya tamko hilo la benki, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata alipinga hatua ya benki hizo na huku Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Profesa Benno Ndulu akisema kwamba benki ziko sahihi kupandisha gharama hizo.
Kwa mujibu wa Kidata , BOT zinapaswa kusimamia benki ili zisiongeze gharama hizo na mamlaka ya mawasiliano (TCRA), kubana kampuni za simu zisipandishe gharama.
Tangu juma lililopita, wateja wa kampuni za simu walianza kuonja chungu ya VAT baada ya kodi, baada ya kuanza kushuhudia wakikatwa fedha kiwango kikubwa zaidi ya ilivyokuwa awali.
Katika mazungumzo na gazeti la Nipashe na watoa huduma za fedha za mitandao ya simu, walisema hata wao walianza kupata malalamiko kutoka kwa wateja kwamba wanakatwa fedha nyingi kuliko ilivyokua mwanzo.
Mmoja wa wateja aliyejitambulisha kwa jina moja la Henry alilielezea Nipashe kuwa alikua anatoa sh. 625,000 kutoka mtandao wa vodacom kwenda Tigo akakatwa sh. 10,500……>>>‘Kwa kawaida ilitakiwa nikatwe sh 7,500 lakini siku ile nilishangaa makato yameongeeka’
Mteja mwingine Hassan Jamal alisema alitumiwa sh. 900,000 kwenye mtandaowa Tigo na alivyotoa alikatwa sh. 8000
Source: Nipashe
Comments
comments