Artists News in Tanzania

Kuvunjika Ndoa ya Rayuu, Mashehe Waingilia Kati

Baada ya uvumi kuwa staa wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ ameachika kwenye ndoa yake ambayo imedumu kwa siku nne tu huku chanzo kikiwa ni familia ya mwanaume, hatimaye mashehe wameamua kuingilia kati kuinusuru ndoa hiyo.

Februari 26, mwaka huu, Rayuu alifunga ndoa na mwanaume mwenye asili ya Kiarabu, Ahmedi Said lakini siku ya nne baadaye ulienea ‘ubuyu’ mitandaoni kuwa alitwangwa talaka tatu kwa sababu ya skendo.

Kutokana na sekeseke hilo lililoacha historia ya kipekee, mashehe mbalimbali walidaiwa kuingilia kati na kuilaumu familia ya mwanaume huyo kuwa ilienda kinyume na matakwa ya Kiislam.

Kwa upande wake, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar, Alhad Mussa aliliambia gazeti hili kuwa ni jambo la ajabu kufanywa na Waislam kwani katika dini ya Kiislam, sababu iliyoainishwa kwenye talaka hiyo haina uzito wa kumfanya aachike kwa sababu walipaswa kubaini hayo kabla ya ndoa hivyo kuitaka familia hiyo kuweka mambo sawa haraka.

Rayuu yeye alisema kuwa alisikitishwa na mwanaume huyo ambaye alimwambia kuwa familia ndiyo iliyoamua iwe hivyo.

Chanzo: GPL

 

Comments

comments

Exit mobile version