Kwenye Muziki Uchawi Upo -Said Fella
Meneja wa Kundi la Yamoto Band Said Fella ‘Mkubwa Fella’ amesema anakubali kwenye tasnia ya muziki hapa nchini uchawi pia upo.
Fella ameyasema hayo katika kipindi cha eNews kinachorushwa na EATV siku ya Jumatano baada ya msanii wa bendi ya Jordan inayopiga nyimbo za injili kusema kwamba kwenye muziki wa Bongo Fleva masuala ya ushirikina yapo sana.
”Ukimtumikia Mungu unakuwa hata ukipata hela yako unajua unaifanyia nini na inakuwa inadumu lakini ukitumikia muziki wa kidunia wengi wanalogana na ndiyo maana mtu anavuma kidogo baada ya muda anapotea kabisa”-Amesema Daniel wa Jordan Band.
Katika kupima kauli hiyo kama ina ukweli ndani yake mtayarishaji wa eNews akaamua kumsaka Diwani wa Kata ya Kilungule Wilayani Temeke Jijini Dar es salaam Said Fella ambaye pia aliunga mkono kauli hiyo.
eatv.tv