Lamata Ataka Waongozaji wa Filamu Wapewe Umuhimu
LEAH Mwendamseke ‘Lamata’ anasema kuwa tasnia ya filamu ina changamoto kubwa sana hasa pale ambapo unakuta watayarishaji wanawatambua na kuwapa nafasi wasanii kuliko hata waongozaji, waandishi wa muswada au watendaji wengine katika tasnia ya filamu.
Inashangaza sana sisi ambao ndio watendaji wakuu hatuthaminiwi kama wasanii wanaonekana katika kamera lakini hakuna msanii mnzuri bila Director au script nzuri lazima tuwe kama wenzetu wa Hollywood.
Lamata ambaye ni mahiri sana uandishi wa mswada wa filamu na muongozaji anaona kuwa kuna utofauti mkubwa na nchi zilizoendelea katika masuala ya filamu kwani watu kama waandishi wa muswada na waongozaji ndio wanaopewa kipaumbele katika uuzaji wa filamu na si wasanii.
fc