Kupitia kipindi cha XXL cha April 20 2017 rapa ambaye alitamba na Nako 2 Nako na WEUSI kutoka Arusha, Lord Eyes ameelezea sababu za kutokuwa karibu na WEUSI akisema waliungana bila mkataba kwa sababu za kimuziki na kutanua wigo wa msanii.
Pamoja na hayo Lord amesema WEUSI ni kampuni na kundi ingawa kumekuwa na utengano, jelause na ubinafsi, lakini hata hivyo amepata baraka zote kutoka kwa watu wake wa Arusha kuwa wamemtuma aje kupiga kazi na asibabaishwe na mtu>>>”Weusi ni kampuni na kundi, ndio mana kumeanza kuwa na utengano, jelause (wivu) na ubinafsi. Kila mtu alikuwa anapata share yake ambayo ameifanyia kazi. Arusha kumekuwa na mitazamo tofauti tofauti, lakini yote kwa yote wanataka baba la baba nipige kazi na mtu asinichengue.” – Lord Eyes.
Kuhusu kutoa wimbo na mahusiano baina yake na Ray C, Lord Eyes alisema:>>>”Mimi nimetoa wimbo, sijui hata Ray C ametoa wimbo lini. Tulishakutana tukapeana mikono japo Ray C wa zamani, pia ana tofauti. Kwa hiyo kabadilika, labda Ray C mpya, kwa sasa hivi nipo kwenye relation (mahusiano).” – Lord Eyes.
Millardayo.com
Comments
comments