WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametoa waraka akisema kitendo cha askari wa Jeshi la Polisi kuwakamata wakati wakiwa kwenye kikao cha ndani cha Chadema jana kimemuimarisha na kumpa nguvu zaidi ya kudai demokrasia.
Katika waraka wake kwa vyombo vya habari leo, Lowassa amesema anafurahishwa na kutiwa moyo na jinsi Watanzania walivyoipokea operesheni yao ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta) iliyopangwa kuanza kesho kwa maandamano na mikutano, lakini vitendo vya polisi vinawapa wasiwasi wananchi.
Lowassa, akiwa na Freeman Mbowe, ambaye ni mwenyekiti wa Chadema, John Mnyika (naibu katibu mkuu-Bara) na viongozi wengine wa chama hicho kikuu cha upinzani walikamatwa jana wakiwa kwenye kikao cha ndani kilichofanyika Hoteli ya Girrafe na baadaye kwenda kituo kikuu cha polisi kwa mahojiano kabla ya kuachiwa na kutakiwa kwenda kituo hapo kesho.
Chanzo:GPL
Comments
comments