Muuza sura kwenye video za Kibongo na msanii mpya wa bongo Fleva, Lulu Abbas maarufu ‘Lulu Diva’ amefunguka na kuweka wazi kuwa aliamua kumuacha rapa Nay wa Mitego kutokana na tabia zake za hapa na pale.
Lulu Diva aliyasema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo ya EATV na kudai kuwa alimua kufikia maamuzi hayo kutokana na tabia za Nay wa Mitego kutotulia na mtu mmoja na kuwatolea tolea macho wanawake.
“Niliamua kumwaga Nay wa Mitego kwa kuwa hajatulia, akiona kila mwanamke macho yanamtoka na kumuwaka, ila naweza kumzungumzia kuwa Nay wa Mitego ni mtu poa sana ukimuona kwenye TV na maisha anayoishi yuko tofauti sana, msafi sana, anajali ni mshikaji poa na ni mtu muelewa sana ila tu ni mtata sana na hizo tabia zingine za kibinadamu ambazo mimi zilinishinda na kuamua kumuacha” alisema Lulu Diva
eatv.tv
Comments
comments