Mshindi wa tuzo ya AMVCA 2016, Elizabeth ‘Lulu’ Michael amefunguka na kuelezea mahusiano yake na CEO wa EFM, Dj Majay baada ya hivi karibuni kuonekana kuwa karibu zaidi.
Akizungumza katika kipindi cha Friday Night Live cha East Africa Television Ijumaa hii, Lulu alisema kama ni kweli yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na Majay basi mashabiki wake watasikia taarifa za ndoa.
“Ninaweza nikasema ndio wakati sio kweli na ninaweza kusema hapana wakati ni kweli, lakini kikubwa zaidi kimaadili ya kitanzania, kimaadili niliyofundishwa mimi, mchumba hatangazwi, ndoa ndiyo inatangazwa,” alisema Lulu.
Aliongeza, “Kama ni kweli ndoa itakuja na watu wataona, lakini siwezi kutangaza wakati bado hatuna mikakati ya ndani zaidi.”
Bongo 5
Comments
comments