Lulu Anaweza Kuwa Mkulima – Mama Lulu
MAMA wa mwigizaji, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila amefunguka kuwa kama si filamu, mwanaye angeweza kuwa mkulima kama yeye au mwandishi wa habari.
Mama Lulu alifunguka hayo hivi karibuni baada ya mwanahabari wetu kumuuliza kuhusu kutoonekana kwa binti yake katika anga la filamu ndipo aliposema kuwa hakumzaa Lulu kuwa muigizaji na anaweza kufanya shughuli nyingine tofauti na sanaa.
“Nilimzaa Lulu awe mkulima kama mimi au mwandishi. Si lazima awe muigizaji kwamba ndiyo na sisi tutaishi. Kazi yoyote atafanya na hategemei filamu ili aishi,” alisema mama Lulu.
Chanzo:GPL