-->

Lulu Atimua Mbio Mahakamani, Baba Yake Atoa Povu

MUIGIZAJI wa Bongo Movie, Elizabeth Michael ‘Lulu’, ametimua mbio katika viunga vya Mahakama Kuu Kanda Maalum ya Dar es Salaam alipokuwa amekwenda kwa ajili ya kusikiliza muendelezo wa kesi yake ya kuuwa bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Charles Kanumba.

Lulu aliwakimbia waandishi wa habari waliokuwepo mahakamani hapo huku baba ake mzazi aliwazuia waandishi wa habari kumpiga picha Lulu.

ukio hilo lilitokea baada ya shahidi wa pili upande wa utetezi ambaye ni mke wa Dk Slaa, Josephine Mushumbushi, ambaye ameshindwa kufika mahakamani hapo leo kwa ajili ya kutoa ushahidi wake kutokana na sababu zilizoelezwa kuwa yupo nje ya nchi (Canada) na hakuweza kupatikana moja kwa moja.

Baada  ya Lulu kutimua vumbi, baba yake naye alikuwa nyuma yake huku waandishi wa habari wakiwafukuzia angalau wapate picha ya tukio hilo hadi kwenye gari analolitumia mwanae na kukaa mbele ya gari kuwaambia waandishi waliokuwepo hivi “Leo picha hampigi tafadhali mwizi amekata kata watu na viroba hampigi picha, mmechimbia chini, huyu mnamfuata, leo hampigi picha hapa,”hayo ndio baadhi ya maneno yaliyosikika kwa Baba Lulu.

Hata hivyo mashabiki wa msanii huyo walianza kuwalaumu waandishi wa habari, kwa kusema kuwa” Kwa nini mmetuondolea Lulu wetu ilibaki kidogo aanguke na angeanguka mngempiga picha mngetukoma,” hayo ni maneno ya baadhi ya mashabiki wa msanii huyo kwa waandishi wa habari.

Mrembo huyo wa filamu anakabiliwa na kesi ya kumuua aliyekuwa mpenzi wake, Steven Kanumba tukio linalodaiwa kufanyika mwezi Aprili mwaka 2012.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364