Lulu Diva Afunguka Kuhusu Kufunga Ndoa
BAADA ya staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kufunga ndoa na Uchebe, msanii anayekimbiza na Ngoma ya Give It To Me, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amefungukia upande wa maisha yake kwamba acha waoane wao lakini kwake noo!
Akizungumza na Showbiz, Lulu aliyewahi kuwa muuza nyago kwenye video za Kibongo alisema kuwa, hafikirii maisha ya ndoa wala kuwa na uhusiano na staa Bongo kwani atapata presha tu.
“Kama kuoana acha waoane wao lakini kwangu noo! Nimeingia kwenye muziki kwa hiyo focus yangu yote ipo hapo, sijawahi kufikiria hata kuwa na mpenzi msanii,” alisema Lulu Diva.