Tunajua ni Watanzania wawili walishinda tuzo mbili kwenye usiku wa tuzo za Africa Magic Viewer’s Choice Awards, wa kwanza ni Single Mtambalike ‘Richie’ na Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambapo Richie tayari alisharudi nyumbani Tanzania usiku wa March 6 2016 ila Lulu hakutokea Airport japo baadhi ya watu walimtarajia.
Lulu alishindwa kutokea jana akiambatana na Richie na kuiambia millardayo.com kwamba hakuweza kurudi hiyo jana sababu alibaki Nigeria kwa ajili ya kazi, kuna watu alikua na maongezi nayo kwenye nchi hiyo maarufu kwa filamu Afrika.
March 7 2016 Lulu amewajulisha Watanzania kwamba anarudi nyumbani siku ya March 8 2016 na atatua uwanja wa ndege Dar es salaam na akayaandika haya
‘Tukijaaliwa uzima…kesho saa 8:30 (saa nane na nusu Mchana) nitaingia uwanja wa ndege Dar Es Salaam na mzigo wenuau acha niseme Tuzo Yenu..!!Can’t wait to see y’all
(I’m hungry and I’m ready 4 change….TODAY)
MillardAyo.com
Comments
comments