Lulu:Nimekataa Dili Kadhaa Kutoka Nigeria
Msanii mahiri wa filamu Bongo, Elizabeth ‘Lulu ‘ Michael amefunguka kwa kudai kuwa tangu alipopata tuzo ya AMVCA 2016 amekataa dili kadhaa kutoka kwa wasanii wa muziki wa Nigeria.
Muigizaji huyo ameitaja sababu ya kukataa dili hizo imetokana na yeye si mwanamuziki wala video vixen.
“Nimepata dili kama mbili tatu kutoka Nigeria za kuigiza filamu na kuna wengine walidhani nafanya muziki,” amekiambia kipindi cha Clouds E cha Clouds TV.
“Nimeshatafutwa na wanamuziki wa Nigeria ambao wengine walitaka niimbe na wengine nitokee tu kwenye video zao, siwezi nikawataja,” alisema.
March mwaka huu, Single Mtambalike (Rich Rich) na Elizabeth Michael (Lulu) walishinda tuzo za African Magic Viewers’ Choice Awards (AMVCA2016) zilizotolewa nchini Nigeria.
Bongo5