Mtoto mzuri katika tasnia ya sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameapa kuwa muda wa kuanza kuzaa ukifika, atazaa mfululizo bila kupumzika hadi lengo la idadi ya watoto anaowataka litimie.
Akizungumza na Bongo Movies ya Amani, Lulu alisema hakuna kitu anachokipenda kama watoto hivyo atakapojipanga na kuwa tayari kuzaa, itakuwa ni bandika bandua kwani anataka kuwa na watoto wengi.
“Jamani hakuna kitu kizuri kama kuzaa kwa kubandika na kubandua, yaani nikimwangalia Mercy Johnson wa Nollywood nchini Nigeria jinsi alivyozaa, napenda sana na ndiyo maana hata mimi wakati wangu ukifika hakuna kupumzika,” alisema Lulu.
Chanzo:GPL
Comments
comments