Artists News in Tanzania

Lungi Maulanga, Achezea Kichapo ‘Hevi’ Kutoka Kwa Mpenzi

Muigizaji wa kitambo Bongo, Lungi Maulanga, anadaiwa kuchezea kichapo ‘hevi’ kutoka kwa mpenzi wake wa zamani (jina linahifadhiwa), kisa kikiwa ni kumnyima unyumba baada ya kukutana baa na kumtaka waondoke pamoja.

Chanzo makini ambacho kilishuhudia mtiti huo kilidai kwamba, Lungi, akiwa anapata kinywaji kwenye baa moja maeneo ya Kinondoni, jamaa huyo aliibuka ‘from no where’ na kuanza kulazimisha watoke eneo hilo, lakini msanii huyo alikataa ndipo ukaibuka ugomvi mzito.
Ilidaiwa kuwa, awali wawili hao walianza kurushiana maneno makali na yalipozidi ndipo Lungi akachezea kipigo kikali cha ngumi na mateke.

“Huo ndiyo ubuyu wa mjini, Lungi alipigwa vibaya kiasi kwamba ukimuona utagundua tu maana ameharibiwa ile sura yake, hasa usoni. “Yule bwana aliyembonda inadaiwa waliwahi kuwa na uhusiano.

Ukweli ni kwamba ugomvi ulikuwa mkubwa sana na baada ya hapo, Lungi alikwenda kutibiwa kwenye Zahanati ya Mwembeni (Kinondoni) kwa siri kwani aliogopa kwenda polisi kwa madai kuwa sakata lingekuwa kubwa na mpenzi wake wa sasa angejua,” kilivujisha chanzo hicho.

Chanzo hicho kiliendelea kutiririsha ubuyu kuwa, kwa sasa jamaa aliyempiga anahaha kuhakikisha Lungi haendi mbali kwani anahofia kazi yake kwa sababu yuko kwenye idara nyeti serikalini.

“Jamaa anamsaka Lungi kwani hajui kuwa hata Lungi hataki ishu iende mbali kwani siku hiyo alimtoroka jamaa yake,” kilimwaga ubuyu chanzo hicho kwa sharti la kutochorwa jina gazetini.

Baada ya kunyetishiwa ubuyu huo, Wikienda lilimwendea hewani Lungi kwa lengo la kupata mzani wa habari hiyo lakini alidai kuwa hayupo nyumbani kwake na kwamba yupo hospitalini kucheki malaria.

MSIKIE LUNGI  

“Jamani sipo nyumbani, najisikia vibaya nimekuja kucheki malaria, nikirudi nitakuambia uje kwani una shida gani na mimi?”alihoji Lungi.

Wikienda kama kawaida yake, lilifanya jitihada za kuthibitisha ubuyu huo ambapo lilitimba nyumbani kwa Lungi maeneo ya Kinondoni kwani hakujua kuwa Wikienda lina ubuyu ambao angeambiwa kwenye simu, bila shaka angeshtukia na kutunga uongo kama wafanyavyo baadhi ya mastaa.

WIKIENDA NYUMBANI KWA LUNGI

Lilipotimba nyumbani hapo, Wikienda liligonga mlango ambao ulifunguliwa na dada ambaye hakujua kuwa ni waandishi wetu hivyo aliwakaribisha nao walitinga moja kwa moja sebuleni na kumkuta Lungi akiwa amejaa tele. Hata bila kuambiwa, waandishi wetu walimshuhudia Lungi akiwa na majeraha ambapo alijikuta akitaharuki na kukosa pa kukimbilia ndipo akawasikiliza walichotaka.

AULIZWA KULIKONI

Lungi alipoulizwa kulikoni kuchezea kichapo, alipangua vikali na kudai kuwa alipigana na kaka yake nyumbani kwao, kisa kikiwa ni mali za baba yao ambapo kesi ipo mahakamani. “Jamani watu wananizushia, majeraha haya ni kwa sababu ya kupigana na kaka yangu achezea kichapo!

LUNGI

Kisa kunyima unyumba… kwa sababu ya mali za watoto wa kambo. Kutokana na utetezi wangu kwa watoto hao ndiyo maana akanipiga,” alisema Lungi.

Pamoja na utetezi huo, kwa kuwa waandishi wetu walikuwa na uhakika kwamba alitwangwa na aliyekuwa bwana’ke, walimbana Lungi sababu ya kuficha na kudai kuwa amekwenda kucheki malaria na hayupo nyumbani, alijibu kuwa hakutaka habari hizo ziandikwe kwa sababu za kifamilia zaidi. “Niliona haya mambo hayafai kuyaweka wazi ndiyo maana nikawadanganya sipo nyumbani,” alijitetea Lungi.

 KAKA WA LUNGI AFUNGUKA 
Ili kuuchimba ubuyu huo, Wikienda lilimtafuta Risasi Maulanga, kaka ambaye Lungi alidai yeye ndiye aliyepigana naye ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Huyo Lungi alipigwa kwenye uhuni wake, akamdanganya baba mtoto wake kuwa mimi nimempiga.

Huo siyo ukweli kabisa na suala hili nitalifikisha kwenye mikono ya sheria ili kumkomesha, aache tabia za kuichafua familia. “Unajua Lungi kutunga uongo kwake ni jambo la kawaida kabisa, nitahakikisha nimemfungulia mashitaka. Kama mnataka kujua ukweli waliulizeni wanafamilia, huyo alipigwa na bwana’ke mwingine.

Sasa ili kuweka mambo sawa ananisingizia. “Hivi nitampigaje wakati suala hili lipo mahakamani? Naomba mchunguze sana suala hili.”

 KUTOKA KWA MHARIRI

Lungi anapaswa kuwa mkweli na kama ana tabia ya uongo kama walivyo baadhi ya mastaa wengine aache mara moja kwani itamfikisha pabaya. Pia ni vizuri akamaliza tofauti zake za kifamilia na kama kuna ugomvi wa mali, aacha mahakama ifanye kazi yake.

Chanzo;GPL

Comments

comments

Exit mobile version