Msanii wa hip hop Roma Mkatoliki amefunguka na kusema kuwa kitendo cha yeye kutangaza rasmi kuoa na kuweka wazi mahusiano yake kimemfanya agundue kuwa mabinti wengi walikuwa wanataka kuwa na yeye kimapenzi.
Roma Mkatoliki amesema hayo alipokuwa akipiga stori kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio na kusema alipoweka wazi baadhi ya picha za Sendoff ya Mama Ivan baadhi ya mabinti wamefikia hatua ya kutotaka kufahamu taarifa zozote kutoka kwa msanii huyo na wengine wamefanya maamuzi ya kum-Unfollow Instagram ili wasione taarifa zozote juu yake.
” Unajua ndoa ni Sacrifice ndio maana saizi vijana wengi wanaogopa kuoa, kwa sababu unapoingia kwenye maisha ya ndoa lazima uta expose maisha hayo na kama unavyojua sisi wasanii tuna mashabiki wa jinsia tofauti, ila tukio la juzi limefanya baadhi ya mashabiki wa kike wanaopenda muziki wangu kuni-Unfollow sababu wapo wengine walikuwa wana tamani siku moja waje kuwa na Roma Mkatoliki faragha hata kama nafanya muziki wa hip hop kama wengi wanavyofikiri, hivyo unapoweka mahusiano wazi kama hivi mtu anaona kama ameikosa ile nafasi hivyo anakuwa disappointed,
Mfano sendoff ya Mama Ivan imefanyika juzi tu hapa lakini nikikuonesha idadi ya mabinti ambao wameni unfollow Instgram baada ya picha zile kuonekana utashangaa, ila nadhani wengine wamekata tamaa sababu walikuwa na matakwa yao lakini mambo hayajakuwa vile walikuwa wanataka” Alisema Roma Mkatoliki
Mbali na hilo Roma Mkatoliki amesema yeye ameamua kufanya mahusiano yake yawe wazi na kuamua kuoa sababu tayari amesha sacrifice kwenye maisha ya ndoa.
Eatv.tv
Comments
comments