Rais wa Manzese, Madee amefunguka kwa kumchana rapa Roma Mkatoliki aache tabia yake ya kupenda kuichunguza simu ya mke wake na kuitumia kila mara kwani ipo siku yatakuja kumkuta makubwa asipoangalia.
Madee amebainisha hayo baada ya msanii Roma kudai hamiliki simu ya kiganjani tokea alipopatwa na matatizo ya kutekwa na watu hivyo sasa anatumia simu ya mke wake Nancy kwa kufanya mawasiliano mbalimbali.
“Watu wa kitanga si unajua jinsi walivyo tabia zao za kupenda kukaa na simu za wake zao muda wote, kuangalia angalia mwisho wa siku unaweza ukakuta kitu mule ukanza kuzua ugomvi kwa hiyo Roma acha kutumia simu ya mke wako mshkaji wangu”, alisema Madee.
Pamoja na hayo, Madee aliendelea kufunguka kwa kubainisha baadhi ya mambo baina yake na familia ya Roma Mkatoliki na kusema amekuwa mtu wao wa karibu sana japo watu wa nje hawafahamu hilo.
“Watu wanatakiwa watambue sisi ni wanamuziki pia watu wa kawaida, Roma pamoja na familia yake yote ni watu ambao tunataniana muda wowote na sehemu yoyote ile. Sasa watu wa nje ndiyo wanakuwa hawajui halafu wanaanza ku-panic”, alisisitiza Madee.
Kwa upande mwingine, Madee amesema anajivunia kuwa msanii wa kwanza Tanzania kutengeneza video ya wimbo kwa ‘style ya animation’ huku akijitapa kuwa hata watu wakiiponda lakini yeye ndiyo ameshaweza kuweka historia aliyokuwa anaitaka kwa kipindi kirefu.
eatv.tv
Comments
comments