MTAYARISHAJI na mwigizaji wa filamu Swahilihood Jimmy Mafufu anayegombea kuwa mwenyekiti wa TDFAA- Taifa amefunguka moja ya mambo muhimu ambayo yanachelewesha kuleta ukuaji wa tasnia ya filamu kwa ukosefu wa Vyuo na kwake ndio kipaumbele chake cha kwanza.
Akiongea na FC Mafufu amesema kuwa kuna mambo mengi lakini kwake amegundua lazima elimu kwa kwanza kwa waigizaji wote kwa nchi nzima hivyo amepanga kuwa na vyuo vitani vya uigizaji kwa muda ambao atakuwa madarakani TDFAA Taifa.
“Nathubutu kusema kuwa chama kilikosa muendelezo na kuwakusanya waigizaji wakae pamoja naahidi kujenga umoja wa kweli na huu utapatikana kwa wasanii wote kujiunga na chama kama kuna mtu hatofanya hivyo nikishinda hatoigiza katika filamu hapa Bongo,”anasema Mafufu.
Pia anasema kuwa atahakikisha anajenga mfumo bora kabisa ambao utajenga heshima na kuwa kazi zilizo bora kabisa huku wasanii wakijenga heshima kuanzia kazi zao na wao wenyewe na kuwa na alama kuu kutambuliwa na taasisi za juu sambamba na Jamii nzima.
Hivyo Jimmy Mafufu amedhamiria kujenga ushirikiano mkubwa sana Wadau wa filamu yaani, Maproducer, Directors, na kila mdau anayehusika na tasnia ya filamu ataheshimiwa na kupewa ushirikiano kwa waigizaji wote bila kubagua yeye ni kiongozi wa wote.
FC
Comments
comments