Mama Afunguka Aunt, Iyobo Kuachana!
MAMA aliyejitambulisha kuwa ni mama mzazi wa dansa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’ Moses Iyobo, amefungukia habari iliyozagaa mitandaoni kuwa mwanaye ameachana na mzazi mwenziye, mwigizaji Aunt Ezekiel kwa kusema habari hizo si za kweli.
Mapema wiki hii, kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, iliandikwa kuwa Moses amemwaga Aunt na kuamua kuondoka nyumbani walipokuwa wakiishi na Aunt maeneo ya Mwananyamala-Kwa mama Zakaria.
Mara baada ya kupata habari hizo kusambaa, wanahabari wetu walimtafuta Aunt bila mafanikio katika simu yake ya mkononi ndipo walipoamua kufunga safari hadi kwenye nyumba hiyo wanayoishi Aunt na Iyobo.
Walipofika, waligonga geti ambapo alitoka mama huyo aliyekataa kujitambulisha jina lake lakini akasema yeye ni mama yake Iyobo na kufunguka kwa kirefu kuhusu taarifa hizo za kuachana kwa mwanaye na Aunt.
“Hizo habari hata mimi nimezisikia. Hazina ukweli wowote. Watu tu wanajaribu kutengeneza uzushi wao kwa maslahi yao wanayoyajua wenyewe.
“Hawajaachana. Ingekuwa kuna ukweli kuhusu habari hiyo, hata mimi usingenikuta hapa. Nipo hapa kwa sababu mkwe wangu na mwanangu wako pamoja sema tu kwa sasa mwanangu Iyobo amesafiri nje ya nchi lakini wapo vizuri,” alisema mama huyo.
Mapaparazi wetu walipoomba kuzungumza na Aunt kuhusiana na habari hizo, mama huyo alisema haiwezekani kwa kuwa amelala hivyo akaomba atafutwe siku nyingine.
Chanzo:GPL