Dar es Salaam. Mama yake, Irene Uwoya, Neema Mrisho amesema hampendi Dogo Janja kwa sababu msanii huyo hana adabu.
Ameyasema hayo ikiwa ni siku chache baada ya Irene Uwoya kusema ameshindwa kumpeleka Dogo Janja kwa wazazi wake, kutokana na kuwa mama yake kuwa mtu wa kusafiri mara kwa mara.
Akizungumza na MCL Digital leo Machi 19, mama Uwoya amesema hata wangeamua kwenda kujitambulisha asingewapokea kwa kuwa Dogo Janja hana adabu ndiyo maana amefunga ndoa bila hata kufuata taratibu.
Akihojiwa mwishoni mwa wiki iliyopita na kituo cha Redio Clouds, Uwoya amesemalicha ya kufunga ndoa tangu Oktoba mwaka jana, hajampeleka Dogo kwa mama yake kwa kuwa ni mtu anayesafiri mara kwa mara huku akiahidi kuwa siku moja watakwenda.
Mama yake, Uwoya amezungumzia utetezi wa mwanaye kuwa hauna mashiko kwani hata kama anasafiri haiwezi kuwa hivyo mwaka mzima na kwamba, ukweli ni mtoto wake anajua wazi kuwa ndoa hiyo hawaitambui na hawamkubali Dogo kwa kuwa ni mtoto ambaye hana adabu.
“Yaani ndugu mwandishi sijui nisemeje na mambo haya sipendi sana kuyaongea kwenye media (vyombo vya habari) kwa kuwa haipendezi kubishana na mtoto uliyemzaa kwenye vyombo vya habari, kwani mwisho wa siku yule ni mtoto wetu tu pamoja na kufanya mambo ambayo hayajatupendezi lakini mwelewe kwamba ndoa hiyo sisi kama wazazi hatuitambui na hatutaitambua,” amesema mama huyo.
Hata hivyo, mama Uwoya amesema ndoa hiyo ibaki kutambuliwa na hao Irene aliowaita kuwa ni ndugu zake, waliokwenda kushiriki harusi yake na waliomfungisha na kwamba, licha ya wazazi kuwa Dar es Salaam, wanashangaa walijitokeza ndugu ambao hawawajui kusimamia jambo hilo.
“Siku ambayo ndoa inafungwa ndugu zake na wazazi wake tulikuwapo lakini tulishangaa kuona kwenye mitandao kuwa amefunga ndoa na hata ilipozidi kuvuma na kumuuliza majibu yake ilikuwa kwamba, alikuwa anacheza movie hivyo tuliamua kuachana nalo kwa kuwa huwezi kumlazimisha mtu akwambie ukweli kwa kile anachokiamini yeye,”amesema.
Mwananchi
Comments
comments