Mambo 9 Kurudisha Soko la ya Kuzingatia Filamu Bongo
KUTOKANA na wasanii wa fi lamu za Kibongo kuwa kwenye mikakati mizito ya kuhakikisha soko la kazi zao linarejea kwenye ubora wake kwa madai kuwa filamu za nje zimeua soko la ndani, kuna haja ya kuyazingatia haya yanayochangia kufeli kwao ili kupaa na kufi kia levo ya kimataifa.
- UBORA WA STORI
Ninapozungumzia ubora wa stori moja kwa moja nawalenga waandishi wa script, unakuta mtu unaamua kuangalia filamu kwa bashasha ukiamini ‘utainjoi’ lakini mambo yanakuwa tofauti, unaitabiri fi lamu mwanzo mwisho na kweli itaenda hivyo.
Mfano unaweza ukasema hapo si kamsaidia lazima atamtongoza na kweli itakuwa hivyo, hapo ataingia chumbani kujifi cha basi itakuwa hivyo, unaweza ukakuta fi lamu nzima itaenda vile unavyohisi utadhani wewe ndiyo umeiandika, tofauti kidogo na fi lamu za wenzetu wanajitahidi kucheza na akili ya kawaida ya binadamu.
- KURUDIA STORI
Kuna stori ambazo zimerudiwa `idea’ aidha kwa msanii mmoja au wasanii tofauti kuiga kazi ya mwenzao, mfano kuna fi lamu ya kaka mkubwa Vincent Kigosi `Ray’ aliicheza miaka ya nyuma, yeye ni mtoto wa tajiri lakini aliamua kuishi kimaskini na kwenda kufanya kazi kwenye nyumba ya matajiri kisha mtoto wa bosi akampenda.
Cha kustaajabisha siku chache zilizopita katoa fi lamu ya kufanana na hiyo ya Geat Keeper na yenyewe, Ray baba yake ni tajiri lakini yeye kaamua kuishi kimaskini na kwenda kufanya kazi nyumba ya matajiri na mwisho motto wa bosi akampenda na kuwa naye, swala hili pia linapunguza mvuto kwa mashabiki.
- KUJUANA
Kuna tabia ambayo inafanywa na wasanii wengi ambayo hata baadhi yao wamekuwa wakilalamikia jambo hilo kuua soko, yaani msanii anavutiwa na muonekano wa mtu f’lani na kuamua kumchezesha kwenye fi lamu yake bila kumfanyisha mazoezi zaidi ya kumpa script aisome basi, matokeo yake anajikuta ‘akimbwela’ kwenye kamera na kuwafanya hata watazamaji wamshtukie na kuchukizwa naye
- MAMBO YA KIZUNGU
Jambo hili linawahusu sana upande wa akina dada, unatazama fi lamu unaandikiwa miaka mitatu nyuma au mbele lakini cha kushangaza nywele ni zilezile zikiwa kwenye msuko uleule tena nywele za bandia, rasta au wigi, wakati nywele hizo haziwezi kusukwa miaka mitatu bila kufumuliwa, ina maana ni uongo wa wazi, pia usiku mtu kalala lakini kajazwa ‘make up’ si sawa.
- KUENDEKEZA UFUSKA
Muda mwingine ubora wa kazi unatoweka kutokana na tabia ya kuendekeza ufuska ‘ngono’ mida ya kazi, wasanii wengi wanapenda kukaa kambini lakini wakifika huko baada ya kuwaza kazi wanawaza mapenzi, hapo utasikia f’lani katoka na f’lani, huyu kamuibia mpenzi yule, basi balaa juu ya balaa matokeo yake muda wa kazi ukifi ka watu wanafanya ilimradi tu siyo kwa kiwango kile walichokikusudia.
- WIVU WA MAENDELEO
Inapotokea msanii kawa juu kuliko mwingine baada ya kuungana na mwenzao ili aweze kufanya vyema zaidi, wanaanza kumjengea chuki na kufanya njama za kumdidimiza, kama wasanii wakongwe kuna msanii anaibuka kwa kishindo basi mpeni sapoti ili afike mbali zaidi huenda akawavuta na nyinyi mkatoboa kupitia yeye.
- UNAFIKI
Kitendo ambacho naweza kusema kinairudisha nyuma tasnia kwa kiasi kikubwa ni hiki, baadhi ya wasanii wanawaza kufi tinishana muda wote yaani hiyo ni moja ya starehe kwao, mtu akiona f’lani na f’lani wanaelewana anawaza kuwachonganisha au wamekaa wanaongea vizuri mmoja akiinuka tayari mwingine anampiga majungu yaani upendo wa kweli ziro.
- USTAA
Kufanya kazi kwa kujiona ni mastaa f’lani kama vile Jacqueline Wolper, Wema Sepetu, Aunt Ezekiel, Jacob Steven ‘JB’, Chuchu Hans, Daudi Michael `Duma’ na wengine hii inachangia kupoteza ubora, sababu baada ya kuwa makini na unachokifanya unawaza tu mimi ni staa f’lani nitatazamwa tu, kazi yangu itauzika tu, siku hizi watu wameeilimika hawajali ustaa wa mtu wanachojali ni ubora wa kazi.
- KUTHUBUTU NA KUJIAMINI
Hili ni jambo la mwisho na la muhimu sana katika kuipeperusha vyema bendera ya nchi yetu, ondokaneni na nidhamu ya uoga changamkeni kutafuta chaneli ya kufanya kazi na wasanii wa nchi mbalimbali, ili kukuza soko letu na kuzidi kuipa sifa nchi yetu, tukaondokana na ile dhana kwamba fi lamu za Nigeria zinapendwa zaidi au za Kihindi au za Kizungu, kwa nini isiwe za Kibongo?
Chanzo:GPL