-->

Man Fongo Sio Mtu wa Kubishana na Mama Yangu-Wema Sepetu

Baada ya kusambaa audio katika mitandao ya kijamii ambazo mama Wema anasikika akimpandishia mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown, Wema Sepetu amemvutia wire mtangazaji huyo akimtaka kuacha kumzungumzia mama yake katika mambo ambayo hayaeleweki.

Wema Sepetu akiwa na mama yake mzazi.

Wema Sepetu akiwa na mama yake mzazi.

Chanzo mgogoro huo mkubwa kati ya Wema Sepetu dhidi ya Christian Bella na Man Fongo kwa pamoja, unahusiana na masuala ya show ambazo ‘design’ wamezungukana na mama ameingilia kati!.

Hivyo Soudy kama kawaida yake aliongea na Man Fongo kujua upande wake wa mkasa huo, lakini alijikuta katika wakati mgumu alivyoamua kumpigia mama Wema ili apate chochote kitu kuhusu ubuyu huyo.

Ijumaa hii Wema Sepetu kupitia kipindi cha U Head, aliamua kumtolea uvivu mtangazaji huyo akimtaka kutomwingiza mama yake katika mambo alioyaita yakijinga.

“Soudy hebu acha kumweka mama kwenye hayo mambo, nakuomba mama yangu sijamuweka kwenye hayo mambo, mama yangu ni mtu mzima namweshimu, nakuomba achana na mambo hayo sijui kumpigia simu, sijui maswala ya Man Fongo, nani anamjua Man Fongo?,” aliuliza Wema. “Man Fongo kweli yule wakukaa kubishana na mama yangu, kwa nini mnamrekodi mama yangu hivyo, mimi sipendi,”

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364