Maneno ya Irene Uwoya kwa Msami ‘Usi-force, panic na yako’
Leo March 20,2018 kwa upande wa burudani story ambayo na yenyewe inachukua headlines ni kutoka kwa mke wa msanii Dogo Janja, Irene Uwoya ambaye leo amechukua dakika zake kuandika Instargram ambapo amem-post staa wa muziki waBongo Fleva ambaye pia ni dancer Msami na kuandika caption ambayo imezua gumzo mtandaoni
Irene Uwoya ameandika…. >>> Mchezaji muziki bora Afrika usi-force ndio kuwa hapana na tafadhali panic kwa hatari yako mwenyewe @msamibaby
Lakini kwa upande wa comments muigizaji Steven Nyerere alionekana ku-comment kutokana na kile ambacho Irene Uwoya ameki-post kwenye page yake ya instagram.
Steven Nyerere ameandika…….>>>“Umeanza tena heee we mwanamke doh leo umemkumbuka tena wewe huyo linda ndoa tushachoka vikao vya ndoa”
Comment ya shabiki anayetumia jina la Killer Platnumz aka-comment na kusema…...>>> “una mume wewe usipost post hovyo waume za watu. Watu watakufikiria vibaya” na baada ya comment hiyo Irene Uwoya alimjibu shabiki huyo.
Kutokana na hichi alichopost Irene Uwoya kwenye page yake ya instagram wengi wameitafsiri kuwa huenda Irene Uwoya na Dogo Janja wapo katika ugomvi na hii ni kwakuwa kuna kipindi tetesi zilisambaa katika mitandao ya kijamii kuwa Msami pamoja naIrene Uwoya waliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi.