KAIMU Mwenyekiti wa Chama cha Maprodyuza Tanzania, William Mtitu, amesema hakuna prodyuza atakayeruhusiwa kufanya kazi ya kutengeneza filamu ndani na nje ya nchi kama hatasajiliwa na chama hicho.
Mtitu alisema chama hicho kimeamua hayo ili kuondoa filamu zisizo na ubora katika soko la filamu nchini ambalo anadai limejaa filamu zisizo na ubora hali inayopelekea kudharauliwa na mashabiki wa kazi hizo.
“Wakati wa kufanya filamu kwa mazoea umepita, kwanza lazima prodyuza awe na elimu ya kazi hiyo kisha asajiliwe bila kufanya hivyo hatopata leseni ya utambuzi wa kuwa mwanachama mwenye sifa za kufanya kazi hizo za uprodyuza wa filamu,” alisema Mtitu.
Mtitu aliongeza kwamba kazi hiyo itaendeshwa bila kuangalia umaarufu wa mtu ama ukongwe wake kwenye kazi hiyo hivyo ni usajili kwa mwaka huu ni lazima ili tuboreshe kazi za filamu na soko lake linaloelekea kuporomoka.
Mtanzania
Comments
comments