-->

Marlaw Apata Mtoto wa Tatu

MKONGWE wa Muziki wa Bongo Fleva, Lawrence Malima ‘Marlaw’ amepata mtoto wa tatu kutoka kwa mkewe ambaye pia ni msanii, Besta Rugeiyamu ‘Besta’.

marlaw

Marlaw Akiwa na Mkewe, zamani

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na wasanii hao ambacho hakikupenda jina lake lichorwe gazetini, Besta alijifungua tangu Novemba 10, mwaka huu mtoto wa kike.

“Kwa sasa wapo na furaha kwa kupata mtoto wa kike waliyemuita Brence. Mtoto wao wa kwanza ni wa kiume anaitwa Starence, wa pili naye ni wa kiume anaitwa Erence,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kunasa ubuyu huo, Risasi lilianza kwa kumtafuta Marlaw aliyewahi kubamba na Ngoma ya Pii Pii (Missing My Baby) ambapo simu yake haikuwa hewani. Alipopigiwa na Besta naye simu yake iliita bila kupokelewa.

Hata hivyo, wasanii wote wawili kupitia kurasa zao za Instagram walithibitisha kupata mtoto wa tatu wa kike waliyemuita jina la Angelina.

“Daah! Leo tuna baraka ya Baby Girl. Thank you God. Amepatikana 10th November 2016 10:37,” aliandika Marlaw.

“Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia kupata mtoto wangu wa tatu salama 10th Nov wiki iliyopita. #Ni Babygal #BabyBrence #BabyAngelina Angelina ni jina la bibi upande wa baba,” aliandika Besta kupitia instagram yake.

Besta na Marlaw walifunga ndoa Agosti 2010. Besta aliyewahi kutamba na ngoma kali kama Kati Yetu, alianza kufifia kwenye gemu baada tu ya kuingia kwenye ndoa.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364