Artists News in Tanzania

Masogange: Natamani Kuwa Mchungaji

UKITAJIWA jina la Agness Jerald na kuambiwa ni muuza nyago kwenye video za Kibongo kidogo unaweza kubishana na mimi lakini ukitajiwa jina la Masogange bila hata kubisha utaanza kuorodhesha video zake alizoshiriki ikiwemo Masogange ya Belle9 pamoja na Msambinungwa ya Tundaman akiwa na Alikiba.

 

Masogange ni mmoja wa modo wasiokauka kwenye midomo ya wanaburudani kutokana na matukio mbalimbali yanayomtokea, ukiachilia mbali suala la kushikiliwa baada ya kuhusishwa na matumizi ya dawa za kulevya, Ijumaa limemfungia kazi maskani kwake, Makongo jijini Dar ambapo amefunguka mengi likiwemo la kutamani kuwa mchungaji;

Ijumaa: Hivi karibuni uliingia kwenye mtihani wa kuhusishwa na matumizi ya dawa za kulevya vipi umeathirika vipi na hiyo hali ya kwenda mahakamani kila mara?

Masogange: Vitu vingi vimekuwa haviendi sawa kwa sababu hata kusafiri haiwezekani tena hivyo mambo mengi yamesimama.

Ijumaa: Najua umetoka kwenye familia ya kidini na hata baba yako ana cheo cha uchungaji, vipi wewe kuhusiana na hilo?

Masogange: (anacheka) Ujue kuna wakati natamani tu hata ningekuwa mchungaji huenda ningekuwa wa kitofauti.

Ijumaa: Na mavazi unayovaa hayawakwazi ndugu zako ambao dini imewakaa?

Masogange: Hapana unajua mavazi hayamfanyi mtu kubadili tabia yake ambayo amekuzwa nayo tangu utotoni.

Ijumaa: Kuna kipindi ulitaka kufanya upasuaji wa kupunguza makalio vipi kuhusu hilo?

Masogange: Hapana kwa sasa nimesitisha hiyo kitu kabisa kuna mtu alinishauri niachane na hilo na nifurahie kile ambacho Mungu amenipa.

Ijumaa: Mastaa wengi wanapenda kutupia picha zao wakiwa na watoto wao lakini kwa nini wewe hujawahi kufanya hivyo angali una mtoto?

Masogange: Upande wa baba yake hawapendi hayo mambo ya kumuanika mtoto kwenye mitandao ya kijamii.

Ijumaa: Sijakuona kwenye nyimbo nyingi na hiyo ndiyo najua ni kazi yako unaendeshaji maisha yako ya kila siku.

Masogange: Siwezi kuitegemea hiyo kazi hata mara moja mimi nina mishemishe zangu nyingine kabisa. Ijumaa: Umri naona kama unaenda bado utaendelea na U-video Queen kwenye nyimbo?

Masogange: Kwenye umri kwenda hamna tatizo maana hata nje ya nchini wadada wakubwa mno wanafanya kazi hii sioni kama kuna tatizo.

Ijumaa: Kwa vile sasa una mtu ambaye ana nia nzuri na wewe kwa nini usiongeze mtoto mmoja.

Masogange: Hapana kabisa hiyo kitu sitaki itokee sasa hivi kabisa maisha magumu mno.

Chanzo:GPL

Comments

comments

Exit mobile version