STAA kitambo kunako Muziki wa Bongo Fleva, Seif Shaban ‘Matonya’ amejitamba kumbadilisha tabia modo mwenye mbwembwe nyingi, Gift Stanford ‘Gigy Money’ kupitia wimbo wake wa Hakijaeleweka.
Akizungumza na Global TV Online kupitia kipindi cha Exclusive, Matonya ambaye aliwahi kuwika pia na vibao kibao kama Teksi Bubu, Vaileth na Anita alisema kuwa, mashabiki wengi wa Gigy Money wamezoea kumuona katika muonekano wa kuvaa nguo ambazo si za kiheshima.
“Nimeamua kumchukua kwa maksudi Gigy katika video hii ya Hakijaeleweka kwanza, wengi wamezoea kumuona akiwa katika mavazi tofauti ya kimitego f’lan hivi lakini kama ukiangalia katika video yangu naweza kusema najivunia kumbadilisha kitu hicho.
“Anaonekana si Gigy yule aliyezoeleka kutokana na kuvaa mavazi ya kiheshima mwanzo mwisho,” alisema Matonya.
Matonya pia aliongeza maana ya Wimbo wa Hakijaeleweka kuwa ni kitendo cha mtu unayekuwa naye kwenye uhusiano bila kujua thamani yake na akiondoka ndiyo unajutia na kuona alikuwa na thamani.
“Kutokengeneza kiitikio ilinichukuwa muda kidogo lakini zipo baadhi ya sehemu ambazo kiukweli hazikuwa gharama sana ila zilitupotezea muda, kwa mfano kuna sehemu ya makaburini ilituchukuwa muda mpaka tumalize taratibu zote za kuchukua kibali kwa ajili ya kutengeneza video humo,” alimaliza Matonya.
Chanzo:GPL
Comments
comments