Mau Anatembelea Nyota za Wasanii
Msanii wa komedi kutoka Bongo Maulid Ali a.k.a Maufundi anatumia mitandao ya kijamii kujiingizia pesa kwa kufanya video kava
Akizungumza na Enewz Mau alisema kuwa kwa sasa amepata staili mpya ya kumuingizia pesa ambayo mara ya kwanza alikuwa anafanya kama burudani lakini amegundua kuwa kupitia hivyo pia anaweza kuvuta mkwanja.
Mpaka sasa Mau ameshafanya video kava za nyimbo kadhaa ikiwemo Jike shupa ya Nuhu Mziwanda na kwetu ya raymond Tiptop huku akiendelea kupokea shavu kwa wasanii wengine.
eatv.tv