Mau Fundi Ahamia ‘Stand Up Comedy’!
MCHEKESHAJI mahiri katika tasnia ya filamu Maulid Ali ‘Maufundi’ amesema kuwa kwa sasa katika kujiongezea kipato kwenye uigizaji anageukia uchekeshaji wa majukwaani (Stand up Comedy) ili kuepukana na hali ya soko la filamu ambalo limepoteza mwelekeo.
“Waswahili husema ukicheka na Nyani utavuna mabua, sasa mimi sitaki kuvuna mabua ndio maana nakimbilia kwingine ambako wengi wanakuogopa kwenye stand up comedy, nipo na Dada yangu Nishabebe,”anasema Maufundi.
Maufundi amesema kuwa baada ya kuungana na mwanadada Salma Jabu ‘Nisha’ mapokeo yamekuwa mazuri sana na kuamini kuwa kazi yake mpya ya kuchekesha katika Majukwaa itawalipa zaidi na inapunguza msongo wa mawazo watengenezapo filamu na kusumbuka kuuza.
Kolabo ya wasanii hawa yaani Nisha na Maufundi imeanza kwa mafanikio katika tamasha lilofanyika Mtwara katika ukumbi wa Makonde (Polisi Mess), baada ya kushangiliwa kwa nguvu wakiwa Jukwaani wakifanya Stand up Comedy.
FC