Muimbaji wa muziki wa injili Emmanuel Mbasha ambaye aliwahi kuwa muwe wa Flora Mbasha amefunguka ya moyoni na kuwamuashia moto aliyewahi kuwa mke wake Flora ambaye siku za karibuni ameolewa na Daudi Kusekwa.
Emmanuely Mbasha amewataka Flora pamoja na huyo mumeo mpya kutoendelea kumtaja taja na kumuhusisha kwenye mambo ambayo yeye hausiki nayo, na kusema yeye saizi ni zaidi ya miaka mitatu imepita toka wameachana hivyo haoni sababu ya wao kuendelea kumtaja taja.
Mbasha inaonekana ametoa povu hili kutokana na kitabu ambacho Flora amekuwa akikiuza kinachozungumzia siri za maisha yake kipindi ambacho yupo na mumewe wa zamani Emmanuel Mbasha, ambacho kitabu hicho kimepewa jina la ‘Siri za Flora Mbasha’.
“Sipendi ujinga kabisa kwani hamuwezi kuuza hicho kidaftari chenu mpaka mtafute kiki kwangu? Acheni hizo mnaniingiza kwenye upumbavu wenu ili mkiuze hicho kidaftari chenu, mbona wengine wanauza vyao kwa utaratibu mzuri, sipendi kabisa mimi naingiaje kwenye hizo ishu za huyo mwanamke miaka zaidi ya 3 siko nae, na ni mke wa mtu na wewe hembu tulia na mmeo huko”. Alisema Mbasha
Mbali na hilo Mbasha aliendelea kuwataka Flora pamoja na huyo muwe wake wasiendelee kumfuatilia kama ambavyo yeye hawafuatilii
“Tena ukome kunitaja taja. Huoni hata haya eti unakiita kidaftari jina langu si ita jina la mumeo huyoo. Kunitaja taja tu taja jina la huyo bwana ako sijui nani vile!!! asinihusishe. Mnikome mbona mie siwafuatili na bwana ako kwa lolote lile, kila mtu apambane na hali yake” alisisitiza Mbasha
Emmanuel Mbasha na Flora walitengana kwa amri ya mahakama na kila mmoja kuanza kuishi maisha ya peke yake, lakini mwanzoni mwa mwezi wa tano mwaka huu Flora aliolewa na mwanaume mwingine anayefahamika kwa jina la Daudi Kusekwa, mwezi mmoja baada ya ndoa Flora pamoja na mume wake mpya ndipo walipo toa kitabu hicho cha ‘Siri za Flora Mbasha’ ambacho kinazungumzia maisha ya Flora Mbasha na yale aliyopitia kipindi yupo na Mbasha.
Comments
comments