Mwili wa mfanyabiashara Ivan Don Ssemwanga ambaye ni mzazi mwenza na mama watoto wa Diamond, Zari the Bosslady aliyefariki Alhamisi hii nchini Afrika Kusini alipokuwa akitibiwa utasafirishwa Jumapili hii kwenda nyumbani kwao Uganda kwaajili ya mazishi kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na familia.
Mjomba wa marehemu, Herbert Luyinda ameviambia vyombo vya habari nchini Uganda kwamba maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu yamekamilika.
“We are in touch with the South African team that took care of Ssemwanga and they booked a Sunday afternoon flight to return the body,” alisema Luyinda.
Baada ya mwili wa marehemu kuwasili Uganda siku ya Jumapili utafanyiwa ibada takatifu siku ya Jumatatu na siku ya Jumanne atazikwa kijijini kwao Nakaliro.
“After church, the body will proceed to Nakaliro village in Kayunga district where he will be laid to rest on Tuesday.”
Mitandao ya Uganda inadai Ivan alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya Shambulio la Moyo (Coronary Artery Disease).
Bongo5
Comments
comments