Msanii kutoka TMK Mh. Temba ambaye sasa hivi anaisimamia kituo cha Mkubwa na wanawe, kwa mara ya kwanza ameweka wazi sababu za ‘Yamoto Band’ kusamabaratika, baada ya kukanushwa mara nyingi na wenyewe kwa muda mrefu wakisema haijavunjika.
Akipiga stori kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Mheshimiwa Temba amesema majungu yaliyopikwa na watu wa nje na tamaa za kuwa na wasanii hao ambao wao wamehangaika kuwatoa kuanzia chini, ndio sababu kubwa ya kundi hilo kusambaratika, kwani kuna watu hao walikuwa wakitamani kuwasimamia wasanii hao mmoja mmoja na sio kundi zima.
Comments
comments