Artists News in Tanzania

Ommy Dimpoz Afunguka Kuhusu Uchawi Kwenye Muziki

Msanii Ommy Dimpoz amesema yeye haamini kama kuna ushirikina, hususani kwa wanamuziki wa bongo fleva.

Ommy Dimpoz ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye stori 3 za Planet Bongo East Africa Radio, na kusema kuwa hawezi kumtuhumu mtu mshirikina kwani hajawahi kumuona mtu akifanya ushirikina.

“Kwenye bongo fleva siwezi kusema kuna ushirikina, au hakuna, mi siamini mambo ya uchawi, siamini ushirikina, sijawahi kukutana nao kwa hiyo siwezi kumtuhumu mtu wala kusema kwamba kuna uchawi, kwa sababu kitu chochote ukikiamini ndo utajua kipo, manaake nikisema kuna ushirikina litakuja swali lingine ok, nani ambaye anafanya ushirikina, na mimi sijui”, alisema Ommy Dimpoz.

Pia Ommy Dimpoz ameongeza kwa kusema kuwa yeye anaamini katika kumuamini Mungu, kwani ndiye mtoa wa riziki na anampa kila mtu.

“Na naamini tu kuna dua kumuomba Mungu, kutoa sadaka ndio vitu ambavyo vinaweza vikakufanikisha, mi naamini kumuomba Mungu, Mungu anampa mtu kile yeye atakacho kwa uwezo wake”, alisema Ommy Dimpoz.

eatv.tv

Comments

comments

Exit mobile version