-->

Miriam Ismail: Kansa ya Bongo Muvi Ni Stori Tu!

KIPAJI chake kimeanza kuonekana alipokuja na filamu ya ‘Best Man’ ambayo iliandaliwa na 5 effect chini ya William Mtitu.  Hapo utajua kuwa binti huyu hakuvamia fani bali hicho ndio kipaji chake alichotoka nacho tumboni kwa mama yake.

Filamu ya Best Man ilizua gumzo nchi nzima kwani alionyesha jinsi gani uhalisia unatakiwa nadhani ingekuwa kipindi hiki basi ni moja ya filamu ambazo zingefungiwa ilionyesha malavidavi ya ndani zaidi ni Mariam Ismail ‘Mama Kubwa’ ambaye anatamba na tamthilia hiyo kama mke mbabe kwa mume asiyejua majukumu ya nyumbani.

Ustaa wake umezidi, uongezeka kwa kasi ya kimbunga kwani uhusikaa ameuwza kutokana na umbo lake kubwa mwenyewe anakwambia yote inatokana na kumsikiliza vizuri muongozaji.

Mariamu anawaambia wasanii wenzake wafanye kazi ili kuweza kumaliza hili ndudumizi la soko la filamu kushuka na kupotea kabisa, kwa kuwa mikakati waliyoiunda kama itatekelezwa basi  hatua watapiga.

Alipokutana na Polisi wa Swaggaz Mariam alisema kuna mambo kama matano inabidi yafanyike ili kuweza kurudisha heshima ya tasnia ya filamu na hakuna mwingine wa kurudisha heshima hiyo zaidi ya wasanii wenyewe wakishirikiana na serikali.

UPENDO

Tuwe na upendo wa dhati baina ya sisi kwa sisi tena wa kweli, kwa kufanya hivyo tutawexza kuambiana kile ambacho maadui zetu wanapanga, maadui zetu ni wanaotoa kazi fake na wasambazaji .

“Mtu akiamuaa kusambaza mwenyewe basi tumpe saport hata kwa kutembea na baadhi ya kazi za mwenzako na kuwonyesha sehemu ambayo unaenda ninauhakika kabisa sisi wenyewe kwa umaarufu tulionao tukipeana saport  basi kazi itafanyika, sio msambazaji wa kizalendo au msanii akianza kusambaza kazi maneno ya anze.”

KUMALIZA KAZI FAKE NA ZILIZOTAFSIRIWA

Sasa hivi wasanii tumeungana na kuanzisha mpango kabambe kwa sababu ya kupoteza kazi za nje zilizotafsiriwa Kiswahili huyu ndiye adui yetu namba moja kwani kazi za nje ambazo zimetafsiriwa zikikomeshwa kuingia nchini watu watarudi kuangalia sinema zetu za hapa nyumbani.

Pili kukomesha cd fake, hili nalo ni jinamizi lililoiangamiza Bongo movie na kutufanya tuishi maisha ya shida kwani wengi wamekuwa wakinunua kazi fake.

Baadhi ya waigizaji wa Best Man

STORY

Pia tuangalie watunzi story zisijirudie  kila muandaaji aiangalie story mara mbili kabla ya kuitumia, kwa sababu hilo nalo linachangia kuuwa soko la filamu.

“Kila mtu sio mtunzi a hadithi ya filamu hilo tunatakiwa tuliangalie kwa umakini, na ndiyo changamoto kubwa sana katika  tasnia wameibuka watunzi na waongozaji ambao kiukweli wamekuwa wakibadilisha tu story.”

Tunasema Kanumba amekufa na tasnia sio kweli alikuwa mshindani sana wa story hakuhitaji story aliyotoka nayo mpinzani wake ambaye ni Ray ifanane nay a kwake alitaka atoe  filamu itakayovuta hisia kuliko ya Ray, kwa sasa hakuna fani imevamiwa na hili ndio tatizo.

RUSHWA YA NGONO

Rushwa ya ngono nayo ni moja ya tatizo lililoingia katika kiwanda cha filamu, msichana ili mradi awe mzuri tu basi anachezeshwa filamu hata kama hajui na kuacha watu wenyevipaji.

“Ninachojua mimi story huwa inamtaka mtu sio mtu anataaka story, waandaaji wengi walikuwa hawalioni hili walikuwa wakiendekeza sana rushwa ya ngono ambapo umoja wa wanawake wa Tasnia tumekuja kulimaliza na tumelisimamia kidete kama msichana sio mmoja wa umoja huo mukimchezesha tutahitaji kujua ametokea wapi nah ii imepitishwa hadi na Rais wa shirikisho,  mabinti walikuwa wakii ngia huku kutafuta majina na kuja kuivuruga tasnia.”

Pia umoja wetu umesimamia skendo za wasanii, tutahakikisha kama unavuma kwa skendo utatolewa kwenye chma na hatua nyingine zitachukulia na kibali hicho kimetoka kwa Rais wa shirikisho Simon Mwakifamba.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364