Mkude Simba: Kweli tumeua filamu zetu
MWIGIZAJI aliye pia mchekeshaji mahiri katika tasnia ya filamu za Swahilihood, Mussa Kitale ‘Mkude Simba’ amekiri soko la Bongo Movie limeporomoka na ndio sababu ya wasanii kukimbilia kuigiza tamthilia badala ya filamu.
“Biashara kubwa ilikuwa katika Bongo Movie, lakini kwa wengi wa wasanii sasa imeyumba, mwokozi wetu labda kwa sasa ni tamthilia, sijui itakuwaje kama na huko nako mambo yakiharibika,” alisema Mkude Simba.
Anafafanua kuwa wasiwasi ni kwamba kama filamu ambayo huchukua wastani wa dakika 60 tu imewashinda wengi, sasa kwenye tamthili ya ambayo huchukua hata miezi wataweza kudumu nayo?
Kutokana na hilo anawashauri wasanii waliokimbilia kwenye tamthilia wafanye kazi kwa kujituma ili kulinda soko liweze kudumu kwa masilahi ya kizazi kijacho pia.
Mwanaspoti