Artists News in Tanzania

Monalisa: Afungukia Maigizo ya Jukwaani,Mkombozi wa Filamu za Bongo

WAIGIZAJI wakongwe kwenye tasnia ya filamu nchini Tanzania, Yvone Cherry ‘Monalisa’ na mama yake mzazi, Suzan Lewis ‘Natasha’, wamesema sanaa za jukwaani zitasaidia kipindi hiki ambacho soko la filamu linaonekana kuyumba.

monalisa34

Yvone Cherry ‘Monalisa’ na mama yake mzazi, Suzan Lewis ‘Natasha’

Waigizaji hao walioanza kuigiza jukwaani muda mrefu, walisema hayo baada ya kushirikishwa katika igizo la ‘Mrs Lucy goes to Africa’ lililoonyeshwa juzi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini hapa.

“Tumefurahi sana kushirikishwa katika igizo hili maana kwa muda mrefu hatukufanya maonyesho kama haya ya uigizaji wa ‘live’ hasa kutokana na soko la filamu kuyumba kwa sasa, hivyo uigizaji wa jukwaani utasaidia kukuza soko hilo kwa mara nyingine,” alifafanua Monalisa.

Naye mwandaaji wa onyesho hilo, Tousant Duchess maarufu Lady T, alisema nia ya tamasha hilo ni kuweka utofauti wa usawa wa burudani ndani na nje ya Tanzania kupitia maonyesho ya jukwaani.

“Nimeanza na Tanzania kisha nitafuata nchi nyingine, pia naipenda nchi hii kwa kuwa ina vipaji vingi lakini pia nitawatangazia wengine huko waje kujionea vipaji vilivyopo hapa,” alisema Lady T.

Mtanzania

Comments

comments

Exit mobile version