MUIGIZAJI asiyechuja kutoka Bongo movie Yvonne Cherryl ‘Monalisa’ anasema kuwa anakutana na changamoto ya kutusiwa na hata watu ambao hawamjui wala yeye pia hana mahusiano nao awali ilikuwa ikimsumbua lakini kwa sasa anaamini kuwa watu wa namna hiyo si wa kuwalaumu inawezekana wana msongo wa mawazo.
“Kuna watu wameumbwa kwa ajili ya kuwakwaza wenzao kuna mtu anaingia katika ukurasa wako na kukushambulia kwa matusi hauelewi kosa lako lakini kwangu nawaambia ukimaliza kutukana piga magoti uombe Mungu akusamehe,”alisema Monalisa.
Monalisa anasema kuwa mara nyingi matatizo hayo yanawakuta wasanii au watu maarufu na si rahisi msanii akitusiwa kuhangakia masuala kama hayo wakati anakuwa na mambo muhimu zaidi ya hizo kero ndogo ndogo za kutusiwa, kwani anapotokea mtu kama huyo ni wazi anakuwa hayupo sawa ni kukwepana nao.
Filamucentral
Comments
comments