Mpenzi Mpya wa Wema Afungukia Alichokipata Baada ya Kudai Hamjui Idris Sultan
Model Calisah ambaye anadaiwa kutoka kimapenzi na Wema Sepetu amesema hajawahi kutukanwa kama alivyotukanwa na watu katika mitandaoya kijamii baada ya kudai kuwa hamjui aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Wema Sepetu na mshindi wa BBA 2014, Idris Sultan.
Calisah wiki tatu zilizopita alidai hamjui Idris Sultan kwa kuwa sio mtu wa kufuatilia maisha ya watu wasiomuhusu.
Akiongea na Bongo5 wiki hii model huyo amesema amekuwa alishambuliwa kwa matusi mitandaoni kwa madai amemdharau Idris Sultan.
“Kusema kweli nimetukanwa sana kwenye mitandao ya kijamii,” alisema Calisah. “Watu wanataka niseme namjua wakati simjui, yaani watu wanalazimisha mimi namjua wakati simjui, kila mtu anachagua watu wakuwajua ndio maana mimi nikasema simjui kwa sababu simfuatilii na wala sijawahi kuingia hata kwenye ukurasa wake wa instagram,”
Model huyo ambaye amewahi kutokea kwenye video kadhaa za muziki, amesema hali hiyo ameichukulia kama jambo la kawaida ambalo hutokea katika maisha ya binadamu.
Bongo5